mahakama ya rufani tu( TZCA) ndio inaweza sikiliza na kutoa amri ya pingamizi ya utekelezaji wa tuzo, pale ambapo shauri hilo lipo katika meza yao.
Mahakama inayoweza kuweka stay for execution (pingamizi la utekelezaji) ni mahakama iliyopitisha hukumu au mahakama iliyopelekewa tuzo hiyo kwaajili ya utekelezaji. ila pale ambapo shauri hilo lipo kwenye meza ya Mahakama ya Rufani ya Tanzania ni mahakama hiyo tu ndiyo inaweza kusikilia pingamizi la utekelezaji na si mahakama yoyote ile iliyopo chini yake. kama inavyo elezewa na kanuni/kifungu cha 11 cha kanuni ya mahakama ya rufani, 2009.