Blog faq

TOFAUTI YA DEEP POOL AND KIAPO CHA MAJINA

· Apr 17, 2026 · 3 min read

TOFAUTI YA DEEP POOL  AND KIAPO CHA MAJINA

nini tofauti ya kiapo cha majina na deep pool

watu wengi huenda sehemu tofauti na huitisha au kuitishwa kiapo cha majina au deep pool, au nyaraka zinginezo zenye dhima sawa, pasipokujua matumizi yake na wapi ina hitajika deed pool na wapi inahitajika affidavit of names (kiapo cha majina).


KIAPO CHA MAJINA

kiapo hichi kinatumika kuthibitisha jina hili /hilo ni lako, na ni yamtu mmoja, haibadili utambulisho bali inaelezea nyaraka husika.

kama kuna makosa madogo madogo ya kiherufi. mf. jina nico ila ukakuta umeandika jina niko, hapa utahitaji kiapo kitakachosema Nico na Niko ni mtu mmoja


DEED POOL

inabadilisha utambulisho kabisa kutoka mtu A kuwa B, kisheria,(kukana na kutolitumia tena jina hilo) kwenye nyaraka zote siku zote za usoni kama kwenye pasi ya kusafiria, NIDA (vitambulisho mbali mbali), na nyaraka za kibenki.

mf. jina ni nicodemus kwenye nyaraka A, bali kwenye nyaraka B jina ni Nicholaus, hapa utahitaji deed pool kusema, jina la nicodemus na kama inavyotambulika sitalitumia tena, bali kuanzia sasa nitatumia jina Nicholaus.

HITIMISHO

deed pool inafuta jina la zamani na kuweka jina jipya kabisa.

affidavit of name(kiapo cha majina) unabaki na jina lako lile lile bali ( na hii hutumika kama kuna makosa madogo madogo ya kiherufi.


Related Articles