Mama John was denied her rights on her late husband's properties and custody of her children
Mama John alikuwa mama wa nyumbani mwenye mume mwenye uwezo na maisha yao yalikuwa mazuri kwamba hawakukosa hitaji lolote la msingi, ila siku moja baba john akiwa safarini akapata ajali na kufariki papo hapo, akaacha mjane wa watoto watatu, wakafanya msiba vizuri ukaisha.
Baada ya msiba wakaka kikao cha familia ikiwemo mama john, shemeji zake, wifi zake na mama mzazi wa baba john. Wakamteua mama mkwe wa mama john kama msimamizi wa mirathi na kwenye kuolozesha mali za marehemu ndo mama John anagundua kuwa mali alizochuma mumewe zote kipindi wako pamoja, baba John alizibadilisha majina na kuweka majina ya mama ake kwahyo mke wake hana chochote.
Kibaya Zaidi mpaka watoto wake wakawa wanachukuliwa na bibi yao kwa kigezo kuwa atawalea yeye aliaminiwa na mwanae kwa kuachiwa mali na mwanae badala ya mke wake. Mama john kaja kutafuta msaada wa kisheria kwenye wakili mtandao, msaidie.
Njia
Mama john anatakiwa kuthibitisha kuwa mali zile zilichumwa kipindi wako pamoja na mume wake na baada ya hapo yeye anaonesha mchango wake kwenye upatikanaji wa mali zile kitu kitachomfanya kuwa na haki mali zile.
Mchango unaweza kuwa wa kiuchumi au wa namna nyingne, na kwa kesi ya mama John mchango wake upo kwenye kumuhudumia mume wake aende kazini bila shida na kufanya kazi bila kujali vitu vingine vyovyote nyumbani kwake, kwani mama John anashugulikia shuguli za nyumabi zote na malezi ya watoto, ushauri kwa mume wake kwenye karibia mali zote alizochuma, kumliwaza anapokuwa na mawazo, kumtia moyo na hata kumuombea. Hvyo mama john anasitahili kulithi mali za mumuwe na kulea watoto wake kwani alikuwa mama bora hata kabla ya kifo cha mumuwe.kwa ushauri Zaidi wasiliana na wakili mtandao.