Blog news

Haki ya mwenye Nyumba

· May 13, 2026 · 3 min read

Haki ya mwenye Nyumba

nini mwenye nyumba (landlord) afanye pale mpangaji hajalipa kodi na hapatikani tena.

miongoni mwetu kuna walio na lengo la kumiliki nyumba/ eneo kwa madhumuni mabli mbali ikiwemo kupangisha, iliyo mada yetu ya leo kujadili.

huwa wapangaji hupatikana na hupangisha kwavipindi tofauti tofauti kama mpangaji na mwenye nyumba walivyo kubaliana, lakini kuna wakati mambo yanaenda tofauti na makubaliano hayo kwani mpangaji anaaanza kusua sua katika sakata zima la malipo na muda mwinginge kushindwa kabisa kulipa kodi na hata kutoroka au kwenda kwenye nyumba hivyo kwa kuibia ibia yaani muda usio kuwa rafiki (usiu wakati mwenye nyumba amelala- kama anakaa mitaa hiyo) au hata kutopokea simu ya mwenye nyumba hiyo. hali hii ikitokea nini mwenye nyumba afanye?


leo tunajadili, nini mwenye nyumba afanye pale ambapo kodi yake ijalipwa na mpangaji huyo hapatikani / ajulikani alipo.


kwanza, ifahamike mwenye nyumba anahaki ya kudai kodi yake pale ambapo kodi hiyo imechelewa, kwa kufungua kesi mahakamani ya madai na yakuvunja makubaliano hayo (mkataba).

pili, kwa kuwa mpangaji hajulikani alipo, mwenye nyumba haruhusiwi kabisa kuuza au kuharibu vitu vya mpangaji hovyo hovyo, na akitaka hivyo anatakiwa kufuata utaratibu maalum wa kisheria.

tatu, mwenye nyumba anaruhusiwa kufungua nyumba hiyo na kutazama vitu vilivyoko humo ndani,

NB: mwenye nyumba atatekeleza hatua hii (haki ya kufungua nyumba hiyo) pale tu atakapo kuwepo na mashahidi- serikali za mitaa na polisi, na atajaza nyaraka maalum, na si vinginevyo.

nne, baada ya kufungua nyumba hiyo (chumba) ya mpangaji, mwenye nyumba anapaswa kutunza (kuhifadhi) mali za mpangaji kwa usalama.

Hatua salama :

Kuandika taarifa rasmi.

Kushirikisha serikali ya mtaa.

Kuweka kumbukumbu ya mali.

tano, kupata amri ya mahakama kabla ya kuuza/kuondoa mali, (na kuthibitisha mpangaji huyo hapatikaniki tena)

kuuza mali hizo ili kufidia deni lake (Hii haipaswi kufanywa binafsi bila utaratibu wa kisheria).


sita, kuvunja mkataba wa kupangisha, mwenye nyumba anahaki ya kuvunja mkataba huo wa kupangisha na kumpangisha mpangaji mwingine nyumba/eneo hilo. (Masharti ya mkataba na muda wa notisi lazima izingatiwe).


KUMBUKA: KUPATA USHAURI WA KISHERIA KABLA YA YOTE

  • Epuka kutumia nguvu.
  • Epuka kuuza mali kiholela.
  • Fuata taratibu rasmi ili kujilinda dhidi ya madai ya baadaye.
  • Andaa notisi rasmi.
  • Au fungua shauri Ia madai ya kodi.

USISITE KUTUTAFUTA UKIKWAMA, tupo kukusaidia.


Related Articles