how to secure your estate before your departure
Katika vitabu vyote vitakatifu, iwe ni Quran, Surah Al-Ankabut 29:64, iwe ni bibilia, Waebrania 13:14: au hata hindu gita Bhagavad Gita 15:8: inasisitiza Sisi sote hapa duniani si makao yetu bali tupo safari kuelekea kwa Muumba Mbingu na Ardhi.
Kwa kipindi hichi tulichopewa hapa duniani Mungu hutubarikia kupata mali za kila aina, ambazo sisi tunatamani kuwaachia urithi tuwapendao/ kizazi kijacho.
Kwani katika bibilia takatifu, Methali 13:22: inatusisitiza “Mtu mwema huacha urithi kwa wana wa wanawe...” hivyo Baba/mama bora ni yule anaye waachia kizazi kijacho urithi, Zaidi ya yote quran takatifu Surah An-Nisa 4:9: “Na waogope wale ambao lau wangaliacha nyuma yao dhuria dhaifu, wangehofia kwa ajili yao...” inatuonya katika kitu tunacho waachia wana wetu isiwe dhuria dhaifu.
Kwani watoto wetu hujifunza kutoka kwetu kwa kuwa sisi tu kioo kama inavyo onekana katika hindu gita, Manusmriti 9:31: “Mwana ni kioo cha baba, kupitia kwake baba huendeleza jina na matunda ya matendo yake.”
Hapa dhana ni kwamba mzazi bora huendeleza kizazi na kuwapatia msingi wa maisha bora ambayo sit u malezi bali na njia sahihi ya kufuata na kutunza mali baada ya kutangulia mbele ya haki,
Tunawezaje kuwapa kizazi/ watoto mali tulizo nazo?, ni kwa njia ya urithi, ulio sahihi Zaidi, ili kukwepa migongano au hata ugomvi baada ya sisi kumaliza safari yetu hapa duniani na kuwa na pumziko la amani huko tuendako.
Usiwaze, Usiogope wala usifadhaike tupo kukusaidia. Tembelea tovuti ya www.wakilimtandao.com , mitandao yote ya kijamii tunapatikana kwa wakili mtandao au tupigie au kututumia ujumbe kupitia whatsapp and Normal call au chati nasi kupitia+255 788 339 939. Kwa barua pepe. info@wakilimtandao.com or wakilimtandao@gmail.com