hatua za ununuzi wa Ardhi Tanzania
Tanzania imetengeneza utaratibu maalum wa mtu yoyote yule anaye taka kununua mali isiyo hamishika mf. Ardhi. utartibu huo haujaelezewa tu na sheria ya jamuhuri bali pia na mashauri mbali mbali ya mahakama za Tanzania na kukubalika na wananchi. taratibu hizo hujumuisha zifuatazo:
i. Hakiki mmiliki (verify the owner).
mnunuzi anawajibu wa kuhakiki mmiliki waeneo hilo/ mali hilo anayotaka kununua na asiwe mtu kati kwa namna yoyote ile, ikiwa ni mtu wa katikati awe amepewa Nguvu kisheria (power of attorney) kushafanya jambo hilo na si vinhinevyo.
ii. Hakiki mipaka ya eneo/ mali (Comfim the boundaries).
ni vizuri na kuhakikisha wewe kama mnunuzi unaembea kwa miguu yako mwenyewe mpka eneo la tukio na kwenda pia hadi kwenye mipaka ya eneo hilo yaani kwenye pembe zote mzunguko wa eneo hilo na ukakariri muonekanao wake., kwa ushauri tu usiruhusu mtu akakuonesha na kukwambia Mwisho/Mpaka ni uleee au vingine.
iii. Hakikia matumizi ya ardhi na masharti yake. (land use and conditions)
hapa mununuzi anatakiwa kuhakikisha na kuongeza umakini sana asije akanunua eneo ya barabara kama nyumba ya kuishi kwani atasumbuliwa baadae, au asije akanunua eneo la kilimo/ shamba kama eneo kanisa / makazi au uwekezaji/ uchimbaji wa madini na n.k.
iv. Angalia miundo mbinu na ufikaji wa eneo lako.(infrastructure and accessibility)
katika kipengele hiki mnunuzi anatakiwa kuhakiki, kuwa eneo analo nunua kuna miundo mbinu zote za msingi na eneo hilo halijaingiliwa na wamili wa miundo mbinu hizo., mfano Barabara, Mamlaka ya maji, hospitali na n.k.
v. zungumza na majirani (Ask neighbers)
vi. fahamu malipo na tozo mbali mbali za serikali (know taxes and frees)
vii. unaweza kupiga picha ma mali hilo unayotaka kununua pia.